Dhumuni la taarifa hii ni kuwapa Viongozi wa Kiafrika (wahudumu wa afya ya jamii, mashirika ya afya, wazee, viongozi wa dini, wataalamu wa tamaduni shirikishi, na wengineo) ujuzi na taarifa zinazohitajika ili kusaidia jamii zetu kuwa salama. Matumani yetu ni kwamba taarifa hii itatumika kama mwongozo na nyenzo ya kujibu maswali yoyote kuhusiana na janga la UVIKO-19 pamoja na mambo mengine yanayoweza kutokea ndini na jamii ya Wahamiaji na Wakimbizi wa Kiafrika.